Pakistan na Lebanon wamekubaliana kuimarisha ushirikiano wa kijeshi wakati mazungumzo ya amani ya Mashariki ya Kati yakiendelea kusuasua.
Wakuu wa majeshi wa Pakistan na Lebanon wamekubaliana kuimarisha ushirikiano wa kijeshi baada ya kukutana nchini Pakistan wakati mazungumzo ya amani kuhusu vita vya Mashariki ya Kati yakiendeleakwa kusuasua.
Mkuu wa jeshi la Lebanon Rodolphe Haykal alikutana na mkuu wa jeshi la Pakistan, Asim Munir na viongozi hao walijadili usalama wa kikanda ushirikiano wa ulinzi na njia za kuimarisha mahusiano ya kijeshi kati ya nchi hizo mbili.
Pakistan imekuwa ikifanya upatanishi kati ya Marekani na Iran kumaliza mzozo huo wa miezi kadhaa huku Tehran ikisisitiza kuwa makubaliano yoyote lazima yajumuishe Lebanon ambako Israel inapigana na Hezbollah inayoungwa mkono na Iran.
Wakati huo huo mapigano nchini Lebanon yameendelea kuwa sehemu muhimu ya juhudi za kumaliza vita ingawa Iran na Israel zilisema Jumatatu kuwa zimesitisha mapigano hali bado ni tete.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime