Mkutao Mkuu wa Umoja wa Mataifa unafunguliwa leo Jumanne, Septemba 22, jijini New York, kwa wiki moja ya mikutano kati ya viongozi wa dunia, katika muktadha wa kuongezeka kwa migogoro na kudhoofika kwa Umoja wa Mataifa.
Masuala kama vile Ukraine, Sudan, akili mnemba (AI), au hata magonjwa ya milipuko yatakuwepo kwenye ajenda. Hata hivyo, Mashariki ya Kati inatarajiwa kuwa na uzito mkubwa zaidi katika majadiliano hayo, kufuatia vita na Iran, kufungwa kwa Mlango-bahari wa Ormuz, na mivutano ya kikanda. Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, ameahidi "kulinda kwa dhati" msimamo wa nchi yake kwenye mijadala hiyo.
Ni mkutano mkubwa zaidi wa kidiplomasia wa mwaka huu. Kwa wiki moja, viongozi wa dunia watakutana New York, kando ya vikao vya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, kuwasilisha misimamo yao kwa jumuiya ya kimataifa.