Ushindani wa kiteknolojia kati ya Marekani na China umeingia katika sura nyingine kufuatia sakata linalohusisha kampuni ya Nvidia na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wake, Jensen Huang, lililoibua mjadala kuhusu mustakabali wa teknolojia ya akili unde (AI).
China inakabiliwa na uamuzi wa kuendelea kuagiza chipu za kisasa kutoka Marekani au kuongeza uwekezaji katika uzalishaji wake wa ndani ili kupunguza utegemezi kwa wazalishaji wa kigeni.
Wakati Marekani ikiweka vikwazo vya kuzuia China kupata chipu za hali ya juu kwa madai ya kulinda usalama wa taifa, Beijing inaendelea kuimarisha uwezo wake wa kiteknolojia ili kushindana na Washington.
Sakata la Huang limeongeza mjadala kuhusu mahusiano ya kiteknolojia na kisiasa kati ya mataifa hayo mawili, huku Marekani ikiripotiwa kuandaa vikwazo zaidi vinavyolenga kuzuia kampuni za China kupata chipu za kisasa.
Kwa upande mwingine, China inaendelea kuwekeza katika mifumo yake ya AI na uzalishaji wa chipu za ndani, ikilenga kuimarisha usalama wa taifa na kujenga uwezo wa kujitegemea kiteknolojia.
Hata hivyo, Beijing bado inakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa mashine za kisasa za kutengeneza chipu, huku vikwazo dhidi ya kampuni ya Uholanzi ya ASML vikiendelea kuathiri juhudi zake za kufikia teknolojia hiyo.
Swali lililoibuka kwa wadau wa teknolojia ulimwenguni ni kwamba China itaweza kujitegemea katika uzalishaji wa chipu na kuipunguza nafasi ya Marekani katika teknolojia ya AI, au itaendelea kutegemea teknolojia ya nchi hiyo?