Urusi yaitishia Estonia na vita vya wazi

Urusi imeituhumu Jirani yake nchi ya Estonia kwa kutelekeza kile imedai kuwa vitendo vya kichokozi, ikitishia vita vya wazi dhidi ya nchi hiyo.

Wizara ya mambo ya nje ya Urusi katika taarifa yake imedai kuwa Tallinn, wanachama wa NATO na Umoja wa Ulaya inakaribia kuchochea vita vya wazi.

Tangazo la Moscow limejiri baada ya Tallinn kutangaza mipango yake ya kuufunga mpaka wake na Urusi, na hatua ya Ukraine kushambumia meli ya Urusi katika Bahari ya Baltic.

Wizara ya mambo ya nje ya Urusi ilimuita balozi wa Estonia jijini Moscow na kumpa malalamiko yake kuhusu uamuzi wa nchi yake kufunga mpaka kati ya Urusi na Estonia.

“Mwanadiplomasia wa Estonia kwa mara nyengine tena amepewa taarifa kwamba vitendo vya kichokozi vya aina hiyo ni hatari zaidi na vinakaribia kuzua vita vya wazi na Urusi.” Imesema taarifa ya Moscow.

Moscow pia inaituhumu Estonia kwa kuiruhusu Ukraine kutumia anga yake kutekeleza mashambulio kaskazini Magharibi mwa Urusi, madai ambayo hata hivyo yamepingwa na Estonia.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii