Rais wa Urusi Vladimir Putin ameituhumu Ukraine kwa kuendelea kushambulia viwanda vyake vya kusafisha mafuta, licha ya wito wa Marekani kuitaka isitishe mashambulio ya aina hiyo. Rais Putin aidha amesisitiza kuwa Urusi itajibu mashambulio hayo.
Kwa upande wake, Kyiv inasema itaacha kushambulia miundombinu ya nishati ya Urusi iwapo Urusi na yenyewe itaacha kuishambulia.
Licha ya kwamba mashambulio ya Ukraine dhidi ya Urusi yamepungua kwa kiasi tangu Rais Donald Trump kutangaza makubaliano ya kusitisha mashambulio dhidi ya miundimbinu ya nishati katikati ya mwezi Oktoba, imenzisha tangu mashmabulio tangu katikati ya mwezi uliopita.
Kwa mujibu wa takwimu kutoka vyanzo viwili vya kiviwanda, mashambulio ya droni za Ukraine yamesababisha kukatika mchakato wa kusafisha mafuta nchini Urusi kwa asilimia 45 tangu mwishoni mwa mwezi Oktoba.
Maeneo kadhaa nchini Urusi yameweka vikwazo kwenye uuzaji wa rejareja wa petroli na dizeli kufuatia wimbi jipya la mashambulio ya Ukraine dhidi ya viwanda vya kusafisha mafuta, kulingana na vyombo vya habari vya ndani na mamlaka husika.
Rais Putin amesema kuwa ingawa hali katika soko la ndani la mafuta bado ni ngumu, bei za petroli zimeanza kuimarika baada ya kufikia kiwango cha juu zaidi mwezi Oktoba.