DRC: Mkuu wa jeshi la Uganda atishia kuingilia kati DRC, Kinshasa yataka maelezo

Mvutano mpya wa kidiplomasia umeibuka kati ya Kinshasa na Kampala baada ya mkuu wa jeshi la Uganda (UPDF), Jenerali Muhoozi Kainerugaba, kutoa vitisho vya kuingilia kijeshi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kupitia mtandao wa kijamii wa X.

Mvutano mpya wa kidiplomasia umeibuka kati ya Kinshasa na Kampala. Serikali ya Kongo ilimwita mwakilishi wa ubalozi wa Uganda kufuatia mfululizo wa taarifa kutoka kwa mkuu wa jeshi la Uganda, Muhoozi Kainerugaba. Katika mtandao wa kijamii X, jenerali huyo alitishia kuwasogeza mbele wanajeshi wake hadi katika eneo la Kongo na kuelezea kuunga mkono kwake kusonga mbele kwa kundi la kisiasa na kijeshi linazoongozwa na Joseph Kabila. Kinshasa inalaani matamshi haya kama ukiukaji wa uhuru wake na inataka ufafanuzi rasmi kutoka Kampala.

Mfululizo wa kauli kali hasa umechochea hasira za mamlaka ya Kongo. Muhoozi Kainerugaba anadai, haswa, kwamba wanajeshi wake waliotumwa Kivu Kaskazini, wakiunga mkono jeshi la Kongo katika kuwasakawaasi wa Uganda wa ADF, hawatapinga kundi la waasi wa DRC linaloongozwa na na rais wa zamani Joseph Kabila kuchukuwa udhibiti wa Walikale. Anatishia hata kuteka mji huo ikiwa waasi watachelewesha kuchukua hatua.

Katika taarifa nyingine, Mkuu wa Uganda anadai kusalimu amri bila masharti kwa uwanja wa ndege wa Isiro huko Haut-Uele. Anahalalisha msimamo wake kwa kutaja mapigano dhidi ya ADF, kundi linalohusiana na shirika la Islamic State, na ulinzi wa jamii ya Bahema.

Mtoto huyo wa Rais Yoweri Museveni pia anawashambulia mamluki wa Magharibi waliopo DRC. Wakati huo huo alimsifu Paul Kagame, akisema kwamba Rwanda na Uganda ni "nchi pacha zinazopigana na maadui zao pamoja."

Vielelezo vya kidiplomasia

Kinshasa sasa inahitaji maelezo na hatua za kuzuia matamshi kama hayo kurudiwa.  Serikali ya DRC, kupitia wizara ya mambo ya nje inayoongozwa na Thérèse Kayikwamba, ilimwita mkuu wa ujumbe wa ubalozi wa Uganda mjini Kinshasa ili kutoa maelezo. Hii si mara ya kwanza. Huko nyuma mnamo mwaka 2024, kauli kama hizo za jenerali huyo zilikuwa tayari zimesababisha mvutano wa kidiplomasia.

Alitishia kuwakamata mamluki wa kigeni waliotumwa Goma, muda mfupi kabla ya jiji hilo kuangukia mikononi mwa AFC/M23.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii