Uchaguzi wa mitaa kufanyika Jumatano wiki hii

Wakati huu raia wa Afrika Kusini wakijiandaa kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa Jumatano ya wiki hii, masuala ya huduma za msingi kama vile maji, ukosefu wa ajira na uhalifu yanatarajiwa kuwa ajenda kubwa kwa raia watakaoamua mustakabali wa miji yao.

Katika Miji ya Johannesburg, Cape Town, Pretoria na Durban, wapiga kura wanakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo kukatika mara kwa mara kwa maji na umeme, ukosefu wa ajira pamoja na kutokuwepo kwa makazi ya bei nafuu.

Kwa mujibu wa ripoti ya mamlaka inayohusika na usambazaji wa maji nchini humo, asilimia tatu ya maji hupotea kutokana na kuwepo kwa miundombinu duni na ya zamani.

Kando na changamoto ya maji na umeme, idadi ya watu wasio na ajira jijini Johannesburg imeongezeka hadi asilimia 35.9 kutoka asilimia 33.0 mwaka huu.

Suala la ukosefu wa usalama pia linatarajiwa kuwa kigezo kikubwa wa wapiga kura, matukio ya utekaji nyara, mauaji yanayotekelezwa na makundi yenye silaha yakiendelea kuripotiwa licha ya kupungua kidogo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii