Abdul El-Sayed ameshinda uchaguzi wa katikati ya muhula katika kiti cha seneti katika jimbo la Michigan mnamo Novemba 3–4, 2026, akimshinda mgombea wa Republican, Mike Rogers. Kupitia ushindi huu, atakuwa seneta wa kwanza wa imani ya Kiislamu katika historia ya Bunge la Seneti la Marekani pindi atakapoapishwa mnamo mwezi Januari 2027.
Wakati wa makadirio ya kwanza ya kiti cha useneta katika jimbo la Michigan, wanaharakati wa chama cha Democratic wameshangilia kwa furaha ushindi huo, anaripoti mwandishi wetu maalum huko Ann Arbor, Justine Fontaine, aliyekuwa kwenye baa moja ya watu kutoka jami ya Ireland.
Abdul El Sayed alikuwa akigombea wadhifa kwa mara ya kwanza… Mtaalamu wa magonjwa ya mlipuko, mtoto wa mhamiaji kutoka Misri, na mwanachama wa mrengo wa kushoto wa Chama cha Democratic, alichaguliwa kwa kura nyingi. Jared Guerrero Salinas, Mooja wa maveterani wa Jeshi la Marekani, alimpigia kampeni. "Yeye ni mtaalamu wa kweli, kiongozi mwenye haiba angavu. "Na hiki ndicho hasa tunachohitaji ili kuwakilisha Michigan katika Baraza la Seneti na kusaidia kupigana dhidi ya mfumo wa utawala wa matajiri wachache, " anaelezea.
Bima ya afya kwa wote, mwisho wa msaada wa Marekani kwa Israel
Abdul El Sayed alikuwa akijaribu kuonyesha kwamba angeweza kushinda kwa kufanya kampeni upande wa kushoto, hata katika jimbo lenye mabadiliko ambalo si la Republican wala la Democrat.
Jenny, mstaafu ambaye pia alishiriki kikamilifu katika kampeni, tayari alikuwa na ujasiri kutokana na idadi kubwa ya wapiga kura katika jimbo hilo. "Nina matumaini makubwa. Nilikuwa katika vituo vya kupigia kura siku nzima, na kulikuwa na foleni ndefu kila mahali. Ilinibidi kupiga simu kote jimboni, na kila mahali nilisikia kulikuwa na watu wengi," alisema.
Akimkabili Abdul El Sayed, Mrepublican Mike Rogers huenda alilipa gharama, kwa kiasi fulani, kwa kutopendwa kwa Donald Trump, ambaye alikuja kumuunga mkono hapa wakati wa kampeni.