Mkutano wa Jumuiya ya Madola wafunguliwa Antigua na Barbuda
Viongozi wa Commonwealth wamekusanyika Antigua kujadili biashara, migogoro na mabadiliko ya tabianchi. Fidia kutokana na biashara ya utumwa na ujuzi wa kidijitali kwa vijana pia zimo kwenye ajenda ya mkutano wa siku nne.
Viongozi wa nchi 56 wanachama waJumuiya ya Madola, Commonwealth, wamekusanyika kisiwani Antigua katika mkutano wa viongozi wa serikali unaofanyika kila baada ya miaka miwili.
Mkutano huo unawaleta pamoja viongozi wanaowakilisha watu bilioni 2.7 duniani kujadili changamoto zinazotokana na migogoro, mabadiliko ya tabianchi, biashara na masuala ya ushuru wa kimataifa.
Katibu Mkuu wa Commonwealth Shirley Botchwey amesema viongozi hao wataangazia namna ya kuongeza biashara kati ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola na kuvutia uwekezaji.
Masuala ya fidia kutokana na biashara ya utumwa, nishati mbadala, pamoja na kuimarisha ujuzi wa kidijitali kwa vijana milioni kumi, ni miongoni mwa mambo yanatarajiwa pia kujadiliwa katika mkutano huo wa siku nne katika nchi hiyo ya Antigua na Barbuda.
Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii