Mahakama nchini Kenya imemhukumu mchungaji Paul Mackenzie, kifungo cha miaka 200 jela kwa kosa la kuwauwa watu 191, ambao 190 kati yao walikuwa watoto.
Akiwa na watu wengine 27, Mackenzie alipatikana na hatia ya mauaji hayo kwa kutoa maelekezo kwa wafuasi wa dhehebu lake kuwaacha watoto wao njaa hadi kufa, ili waweze kukutana na Mungu.
Mackenzie ambaye alikuwa mchungaji wa kanisa la Good News, alikamatwa mwaka 2023 baada ya kugunduliwa kwa zaidi ya miili 400 katika makaburi ya kina kifupi katika msitu wa Shakahola, pwani ya Kenya. Tukio ambalo liliibua mjadala mkubwa katika taifa hilo la Afrika Mashariki.