China yazionya nchi za ASEAN kujiepusha kutumiwa

Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi leo ametowa tahadhari kwamba nchi zinapaswa kujiepusha kutumiwa na nchi zenye nguvu katika kanda ambayo iko kwenye hatari ya kubadilishwa kutokana na sababu za siasa za kikanda. Wang Yi ameyasema hayo kupitia hotuba yake ya kisera mjini Jarkata nchini,Indonesia katika mkutano wa sekretariati ya jumuiya ya nchi za kusini mashariki mwa Asia-ASEAN. Wang Yi amesema nchi nyingi katika kanda hiyo ziko katika shinikizo kuchukua upande na kwahivyo zinapawa kujitenga na uhasama na ushawishi wa mataifa yenye nguvu na kuongeza kusema kwamba mustakabali wa kanda hiyo unapaswa kuwa mikononi mwa watu wa kanda hiyo.Nchi za Kusini Mashariki mwa Asia kwa miaka zimekuwa ni eneo la mivutano ya siasa za kikanda kati ya mataifa makubwa kutokana na umuhimu wake wa kimkakati ambapo baadhi ziko kwenye wasiwasi wa kuchagua upande katika suala la uhasama baina ya China na Marekani.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii