Rais wa Sri Lanka anayekabiliwa na shinikizo aondoka Maldives

Rais wa Sri Lanka Gotabaya Rajapaksa leo ameondoka kutoka visiwa vya Maldives alikowasili jana baada ya kuikimbia nchi yake kufuatia shinikizo la maandamano ya umma yanayomtaka kujiuzulu kutokana na mzozo mkubwa wa kiuchumi. Afisa mmoja wa serikali ya Maldives aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina amesema Rajapaksa aliabiri ndege ya shirika la Saudi Arabia inayoelekea Singapore anakotarajiwa kuishi kwa muda. Rajapaksa na mkewe waliikimbia Sri Lanka jana Jumatano wakitumia ndege ya jeshi wakati waandamanaji wakiendelea kuyamakata majengo ya serikali kumlazimisha kujiuzulu wakimtikwa dhima ya kuwa chanzo cha hali mbaya ya kiuchumi inayoikabili nchi hiyo. Hata hivyo inaarifiwa hadi sasa kiongozi huyo hajawasilisha barua yake ya kujiuzulu licha ya kutoa ahadi ya kufanya hivyo jana na badala yake amemteua waziri mkuu kuwa rais wa muda.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii