Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu na wasanii mbalimbali wa Bongo Fleva akiwemo Harmonize, Marioo, Sholo Mwamba, Balaa Mcee, Sarafina, Mimi Mars, Mzee wa Bwax wameungana na umma wa Mtwara kutoa elimu na kuhamasisha matumizi ya chanjo ya UVIKO-19 katika uwanja wa Nyangwanda Sijaona.. Tukio hili limeandaliwa na Wizara ya Afya kupitia kitengo cha Elimu kwa Umma, pamoja na FHI 360 kupitia mradi wa EpiC kwa ufadhili wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID).
Malengo ya nchi ni kuchanja asilimia 70% ya wananchi wake kufikia mwishoni mwaka 2022,
Mpaka kufikia tarehe 10 Julai Mtwara ilikuwa imechanja asilimia 29.3% ya wananchi wake . “Tunashukuru sana Serikali yaawamu ya sita ikiongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassani kwa uamuzi wa kuwalinda wananchi wake dhidi ya Ugonjwa wa UVIKO-19 na magonjwa mengine” alisema Ummy Mwalimu Waziri wa Afya.
Wizara ya Afya kupitia kitengo cha elimu ya Afya kwa umma kwa kushirikiana na wadau fhi360 unatumia tukio la kimuziki la Mziki Mnene likiambatana na kauli mbiu ya “Bega kwa Bega, Ujanja Kujanja” kuongeza kasi ya kutoa chanjo ya UVIKO-19“Kupitia Kampeni hii tunaendelea kukumbushana kukamilisha dozi,
kusajliwa na kupata cheti cha chanjo ili kwa pamoja tufikie malengo ya
kuikinga nchi yetu dhidi ya janga hili. Hivyo, ninawashukuru viongozi na
wananchi wote mliofika hapa hii leo kushiriki uzinduzi huu pamoja na
kuendelea kushirikiana kwa kuhamasishana sisi kwa sisi kutumia chanjo
hizi. Vilevile,
ninawashukuru FHI 360 na USAID Tanzania kwa kuandaa na kuwezesha shughuli hii.” Alisema
Mheshimiwa Ummy Mwalimu. Katika kuonyesha jinsi wadau wa maendeleo
wanavyoshirikiana na serikali kuhakikisha inafikia malengo ya uchanjaji
waliojiwekea na mikoa ambamo kampeni ya Mziki Mnene itatekelezwa,
mwakilishi mkazi wa FHI 360 nchini Tanzania, Waziri Nyoni alisema;
“chanjo ya UVIKO-19 imekuwa ni moja ya mkakati unaotekelezwa kwa
msisitizo mkubwa zaidi baada ya kuzinduliwa rasmi nchini na Mhe. Samia
Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniamnamo Julai, 2021.
Kutokana na juhudi hizi zinazofanywa na serikali kwa kushirikiana na
wadau, kasi ya maambukizi ya UVIKO-19 imeendelea kupungua nchini.
Kampeni ya kuhamasisha chanjo inatarajiwa kufanyika katika mikoa mitano
ambayo ni Lindi, Mtwara, Ruvuma, Njombe na Iringa.”
.