NUSRAT KUHAMIA RASM CCM

Zilianza kama tetesi kisha zikasikika taarifa za kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na baadaye kutumia majukwaa mbalimbali ikiwemo Bunge kupongeza kazi zinazofanywa na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Lakini sasa ni rasmi kuwa Mbunge wa Viti Maalumu Kundi la Vijana Mkoa wa Singida ambaye awali alikuwa kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kabla ya kuvuliwa uanachama kwa kukubali kwenda kuapishwa bungeni Nusrat Hanje amejiunga na CCM.

Hanje ametangaza uamuzi huo kwenye mkutano wa hadhara Mei 19, 2025 uliofanyika viwanja vya stendi ya zamani Ikungi ikiwa ni miezi michache kabla ya Bunge kuvunjwa. Katika mkutano huo, Hanje kama ilivyo kwa makada wengine waliojivua uanachama ndani ya Chadema, amedai kuwa chama hicho kimepoteza mwelekeo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii