SERIKALI YABAINI TAARIFA ZA UPOTOSHAJI

Serikali imebaini uwepo wa taarifa za upotoshaji kupitia mitandao ya kijamii hususani ukurasa wa X kwa kuchapisha maudhui yenye lengo la kuzua taharuki na kuwajaza hofu wananchi.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo Mei 20, 2025 na msemaji mkuu wa serikali inaeleza kuwa  imebainika kuna wahalifu ambao wanafungua akaunti za mitandao ya kijamii yenye majina yanayofanana na taasisi zinazoaminika na kuchapisha maudhui ya upotoshaji na zenye kuzua taharuki.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Serikali inatoa onyo kwa wote wanaofanya uhalifu huo na tayari hatua za kisheria zimeachukuliwa dhidi yao ili kukabiliana na wahalifu hao.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii