Waalimu wa dini ya kislaam mkoa wa Mwanza wametakiwa kuwafundisha watoto na jamii maadili mema na kuipenda Nchii yao.
Hayo yamesemwa na sheikh wa mkoa wa mwanza Hasan Kabeke katika semina iliyoandaliwa na ofisi ya bakwata mkoa wa Mwanza kuwaongezea ujuzi na uwezo waalimu hao.
Sheikh kabeke amesema kuna mambo sita muhimu ya kuzingatiwa katika kufundisha dini na ni lazima yafuatwe ili kupata jamii yenye maadili mema na isiyokuwa na migogoro yenyewe kwa wenyewe.
Wakizungumza baada ya semena hiyo walimu wa dini ya kislaam wamesema mafunzo hayo yamewaongezea uwezo na maarifa zaidi hali itakayo wawezesha kufanya kazi yao kwa ufanisi zaidi.