CHADEMA KUFANYA MKUTANO WA BALAZA KUU MEI 21

Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) inatarajia kukutana jijini Dar es Salaam Jumatano Mei 21, 2025 kwaajili ya kufanya kikao maalumu.

Kikao hicho kimeitishwa mara baada ya kipindi  chama hicho kinapitia wakati mgumu ikiwemo misukosuko  ya mwenyekiti wake, Tundu Lissu kuwa gerezani akikabiliwa na kesi mbili ya uhaini na ile ya kuchapisha taarifa za uongo mitandaoni.

Pia makada na viongozi wake kuanzia ngazi ya kamati kuu, kanda, mikoa, wilaya, majimbo hadi kata wakitangaza kukihama kwa madai ya kuwa kimepoteza mwelekeo wake.

Aidha kamati kuu hiyo imeitishwa wakati ambao Ofisi ya Msajili mkuu wa vyama vya siasa ikiwaandikia barua Chadema ya kuwaeleza kutokuwatambua viongozi wanane wa kamati kuu na sekretarieti.

Hayo yametokana na kudai akidi ya Baraza Kuu la Januari 22, 2025 haikutimia na kuwataka kuitisha upya baraza hilo ikiwa Miongoni mwa viongozi hao ni Katibu Mkuu, John Mnyika na naibu wake wawili Bara na Zanzibar.

Aidha kikao hicho kimeitishwa na Makamu Mwenyekiti  Bara, John Heche katika kipindi  ambacho makada na viongozi wake wanaokikimbia wakieleza wazi kuwa Heche ameshindwa kukiongoza vyema chama kupitia vikao badala yake kimekuwa cha matamko pekee.

Ikiwa siku moja kupita yaani Ijumaa, Mei 16, 2025, Heche alizungumza na wanachama wa Chadema Famili Kijiji cha Kakola wilayani Kahama mkoani Shinyanga katika kikao cha ndani alitangaza uwepo wa kikao hicho.

Amesema kikao hicho kitajadili mambo kadhaa ya ustawi na mikakati ya chama ikiwemo muendelezo wa kampeni ya No reforms, no election 'bila mabadiliko hakuna uchaguzi' ambayo itashirikisha na kufanyika katika kanda mbalimbali za chama hicho.


Bila kutaja ajenda za kikao hicho Heche alisema: Mei 19, 2025  watanaenda Mahakama ya Kisutu kwenye kesi ya Mwenyekiti wetu Tundu Lissu na Mei 21 tutafanya kikao cha Kamati Kuu baada ya hapo tutaueleza umma nini kinafuata Chadema siyo tu ni chama cha siasa, Chadema ni imani katika mioyo ya Watanzania wapenda haki na demokrasia."

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii