Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya ufunguzi wa Daraja la JP Magufuli lililopo Kigongo-Busisi itakaofanyika June 19 mwaka huu.
Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega ametoa taarifa hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza wakati akiongea mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye yuko katika ziarani yake Mkoani Mwanza.
Waziri Ulega amewataka Wananchi wa Mwanza kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa daraja hilo lenye urefu wa kilometa 3 na barabara zake unganishi zenye urefu wa kilometa 1.66 na linalotarajiwa kuwa refu kuliko yote katika eneo la Afrika Mashariki na Kati.
Akiongea katika mkutano huo Waziri Mkuu amesisitiza umuhimu wa Wananchi kujitokeza kwa wingi katika tukio hilo ambalo wananchi walilingojea kwa muda mrefu kutokana na uwekezaji wa kodi na mspato kwa wananchi.