Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Bw. Francis Alfred Mwakabumbe alisema kuwa ingawa bei ya zao la korosho huathiriwa na mabadiliko ya soko dunia kutokana na kuwa zao la kimataifa lakini tanzania ina nafasi ya kipekee kutokana na ubora wa utengenezaji korosho zake.
Akizungumza kuhusu mwenendo wa bei ya korosho Mwakabumbe alisema kuwa Bodi ya Korosho ina jukumu kubwa katika kupanga bei kwa kuzingatia maeneo mbalimbali ingawa kuna changamoto kubwa ambayo inasababishwa na mahitaji ya uhitaji katika soko la dunia.
“Tunachoangalia kama Bodi ni maeneo gani tufanye bei Na ukiangalia duniani Tanzania ndiyo nchi yenye korosho bora kuliko maeneo mengine kwa sababu tunasimamia ubora, na korosho tunayoipeleka sokoni tunaipeleka kwenye viwango vya ubora unaotakiwa,” alisema Mwakabumbe.
Kauli hiyo imekuja wakati serikali ikiendelea na maandalizi ya Bajeti ya Wakulima ikilenga kuhakikisha wakulima wananufaika ipasavyo na mazao yao.