Mkuu wa Wilaya Babati Mkoani Manyara Emmanuela Kaganda amewaonya Madereva wa boda boda wilayani humo kutotumika vibaya na makundi ya wanasiasa wasiokua waadilifu, kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Octoba 2025 na kushiriki vitendo vya uvunjifu wa amani na badala yake wafanye kazi kwa weledi na kutunza amani na mshikamano wa kitaifa.
Akizungumza hayo mara baada ya kukabidhi pikipiki kwa makundi ya vijana ikiwa ni utekelezaji wa mikopo ya asilimia 10, iliyotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Babati.