Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Taifa, Mzee Hashim Rungwe Spunda na Viongozi wengine wa chama hicho akiwamo Kaimu Makamu Mwenyekiti wa CHAUMMA, Devotha Minja tayari wamewasili kwenye ukumbi wa mkutano Jijini Dar es salaam leo May 21,2025 kwa ajili ya Grand Reception.
Rungwe amesema kuwa hakuna maendeleo ya kweli katika taifa linalokabiliwa na changamoto ya lishe duni, huku akisisitiza misingi ya taifa imara ni wananchi wenye afya bora.
Kauli hiyo ameitoa leo Mei 21, 2025 katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam, ambapo chama hicho kimepokea wanachama wapya zaidi ya 3,000, wengi wao wakiwa waliokuwa wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Aidha ametoa ufafanuzi wenye kauli isemayo taifa ambalo halina lishe hakika halitaweza kuendelea na ndio maana sisi Chaumma tunaamini kuwa ili kujenga taifa madhubuti na lenye watu imara ni lazima tuhakikishe kuwa wanapata lishe madhubuti tangu wakiwa watoto na huwezi kujenga taifa imara kama watu wake wanakuwa na shida ya utapiamlo ,"ndio maana halisi ya kauli mbiu yetu ya Ubwabwa kwa wote karibuni tukajenge taifa lililoshiba na lenye afya njema,”
Ili kupata taarifa zaidi endelea kutufuatilia kupitia website yetu ya www.jembenijembe.com kupitia Instagram ,Facebook, tikok,x zamani twitter pamoja na YouTube