MAZUNGUMZO YA TRUMP NA CYRIL RAMAPHOSA KUHUSU MAUWAJI YA WAZUNGU.

Rais wa Marekani Donald Trump alimuuliza Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa pindi walipokutana Ikulu ya White House nchini Marekani May 21,2025 kwamba kama Serikali yake haiungi mkono ubaguzi na mauaji ya Wazungu nchini Afrika Kusini kwanini hadi leo hawajamkamata Kiongozi wa Chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) na Mbunge wa Bunge la Afrika Kusini Julius Malema ambaye alitangaza hadharani mbele ya umati wa Watu kuwa Wazungu wanapaswa kuuawa na kupokonywa ardhi zao.

Trump aliuliza swali hilo muda mfupi baada ya Trump kuagiza TV iwashwe na kimwonyesha Ramaphosa jinsi ambavyo baadhi ya Viongozi na Wanaharakati nchini mwake akiwemo Malema walivyotangaza hadharani kile Trump alichokiita ubaguzi wa Wazungu na kuwapokonya ardhi zao ambapo licha ya kutazama video hiyo Ramaphosa aliendelea kusisitiza kwamba Serikali yake haiungi mkono mauaji ya Watu.

Itakumbukwa katika siku za nyuma Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alimjibu Rais Trump aliyetangaza kusitisha misaada nchini humo kwa madai ya ukiukwaji wa haki za Binadamu kwa Wazungu kunyanyaswa na kupokonywa ardhi wanazomiliki ambapo Ramaphosa alimtaka Trump aache kuingilia  ya Afrika Kusini kwakuwa hayamuhusu na kusema ardhi ya Afrika Kusini sio ya Trump hivyo hakuwa na haki ya kuwapangia cha kufanya.

Mkutano wa Viongozi hao uliitishwa ili waweze kuzimalize tofauti zao na kurejesha ushirikiano mpya ikiwa Trump alimtaka Ramaphosa kukiri kuwa Wazungu wanabaguliwa nchini mwake na alipokataa iliwashwa TV na ushahidi wa nakala nyingine muhimu za karatasi na picha pamoja na video zilizoonesha mashamba ya Wazungu yanayodaiwa kupokonywa nchini humo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii