Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) Itikadi na Uenezi Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) CPA Amos Makalla amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali iliyokamilika ambayo iliasisiwa na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano hayati Dk John Pombe Magufuli kisha kuanzisha miradi mingine mipya.
Makalla ameeleza hayo wakati akizungumza na wananchi katika eneo la Usagara Wilaya ya Misungwi mkoani mwanza akiwa katika muendelezo wa ziara yake ya mikoa mitano ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Kagera, Geita, Mwanza, Simiyu na Shinyanga.
Hivyo amesema kuwa kukamilika kwa daraja la Kigongo -Busisi, mradi wa SGR na meli itasaidia kuchochea biashara na kukuza uchumi wa wananchi wa kanda ya ziwa na ndiyo sababu amepita kueleza jitihada za serikali na kazi nzuri inayofanya katika utekelezaji wa sera mpya ya maendeleo .
Ameongeza kuwa magari kutoka nchi jirani za Kongo na Rwanda yatapita ambayo yatasaidia kukuza uchumi wa taifa na kuongeza uchumi wa nchi.
Pia mradi wa pili ambao Rais Samia aliahidi na kuanzisha ni kuendeleza kipande cha kutoka Dodoma hadi Makutupola kwenda Tabora, Isaka hadi Mwanza na alianza kwa kumalisha kipande kilichokuwa kimebaki kutoka Dar es salaam hadi Dodoma , mradi wa Meli ya MV Mwanza ambayo aliikuwa imefikia asilimia 60 ya utekelezaji wake na aliondoka ikiwa imefika asilimia 98 lakini hadi sasa imekamilika na itafanya safari kuanzia Mwanza, Bukoba hadi Uganda.