Ikiwa ni moja ya kumbukizi zisizoweza kusahaulika kwa Wakaazi wa Kanda ya Ziwa kila ifikapo Mei 21 ya kila mwaka kupoteza wapendwa wao katika ajali ya MV BUKOBA.
Hapo jana Mei 21, 2025 imetimia miaka 29 tangu kuzama kwa meli ya MV Bukoba katika Ziwa Victoria, baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Mwanza wameipongeza Serikali kwa kuboresha usafiri na usafirishaji majini.
Ikumbukwe kuwa Meli ya MV Bukoba ilizama Mei 21, 1996 katika Ziwa Victoria ikiwa katika safari zake za kawaida kutoka Bukoba mkoani Kagera kuelekea mkoani Mwanza na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 800.
MV Bukoba ilikuwa meli maarufu ya abiria na mizigo iliyokuwa ikiunganisha miji mikubwa ya kanda ya Ziwa Victoria – hasa Mwanza, Bukoba, na maeneo ya kati kama Kemondo. Kwa miaka mingi, ilikuwa tegemeo kubwa kwa wasafiri na wafanyabiashara waliotumia njia za majini kutokana na ukosefu wa miundombinu bora ya barabara na reli.
Mnamo tarehe 21 Mei 1996, MV Bukoba ilizama katika maji ya Ziwa Victoria kwa urefu wa takribani kilomita 30 kabla ya kufika Bandarini Mwanza Meli hiyo ilikuwa imesheheni abiria waliotoka Bukoba kuelekea Mwanza, wengi wao wakiwa wametoka kwenye sherehe za kifamilia, harusi na shughuli nyingine za kijamii.
Inakadiriwa kuwa meli hiyo ilikuwa na takriban watu 1,000, ingawa uwezo wake wa kubeba abiria ulikuwa ni watu 430 tu. Hali hiyo ya kubeba abiria kupita kiasi, pamoja na hitilafu za kiufundi na usimamizi mbovu, ilisababisha meli hiyo kuezuliwa na maji na kuzama kwa haraka.
Na hapa kuna idadi ya watu waliopoteza maisha katika meli hiyo Kati ya watu 800 hadi 1,000, ingawa idadi kamili haijawahi kuthibitishwa rasmi.
Ingawa wapo watu baadhi Walionusurika katika ajali hiyo ni Takriban 114, ambao wengi wao wakionekana kusaidiwa na wavuvi waliokuwa karibu na eneo hilo la tukio na kuonyesha kutoa msaada kwa abiria waliokuwa wakiogelea juu ya maji.
Uchunguzi ulionesha sababu kuu zilizopelekea meli kuzama ni pamoja na:
○ Kubeba abiria kupita kiasi (overloading),
• Kutokuwepo kwa vifaa vya kujiokoa (life jackets, boti ndogo)
• Ukaguzi duni wa kiusalama
• Kutokuwepo kwa mawasiliano ya dharura kwa haraka.
Na hizi ni miongoni mwa Athari zilizotokea kwenye ajali ya MV Bukoba na kupelekea il pigo kubwa kwa taifa zikiwemo:
• MV Bukoba Iliwaacha maelfu ya familia katika majonzi makubwa.
• Meli ya MV Ilizua mijadala mikubwa kuhusu uzembe katika sekta ya usafiri wa maji.
• Ilisababisha mageuzi fulani katika sera za usafiri wa majini, ingawa utekelezaji wake bado umekuwa na changamoto kubwa kwa wasafiri.
Katika hayo zipo baadhi ya kumbukumbu, alama na Urithi ulijengeka ndani ya vichwa vya wananchi na taifa kwa ujumla ili kuwaenzi wapendwa wao miongoni mwao ni:
• Mnara wa kumbukumbu kwa waathirika ulijengwa eneo la Igoma jijini Mwanza.
• Kila mwaka, tarehe 21 Mei, familia na wafiwa hukutana kuwakumbuka wapendwa wao.
• Tukio hili limekuwa somo kubwa kwa sekta ya usafiri kuhusu umuhimu wa usalama na udhibiti.
Kutokana na hayo watanzania na wakazi wa Kanda ya Ziwa wakikumbuka tukio hilo sauti za mashuuhuda zilisikika kwa masikitiko na mojonzi mioyoni mwao huku wakikiri kuwepo kwa mageuzi makubwa katika sekta ya usafiri na usafirishaji majini.
Ili kupata taarifa zaidi endelea kutufuatilia kupitia website yetu ya www.jembenijembe.com kupitia Instagram ,Facebook, tikok,x zamani twitter pamoja na YouTube