CWT WATANGAZA NAFASI ZA WAGOMBEA MBALIMBALI

Kati ya wagombea waliojitokeza, 18 wanawania nafasi ya urais huku 19 wakigombea nafasi ya Makamu wa Rais. Makamu wa Rais wa sasa, Ikomba Suleiman, amejiunga katika kinyang’anyiro cha urais na atapambana na Rais aliyepo madarakani, Leah Ulaya, ambaye anawania kutetea nafasi hiyo.

Jina la Leah lilivuma mwaka juzi baada ya Januari 25, 2023 kukataa uteuzi wa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbongwe, mkoani Geita, aliopewa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Pia, aliyekuwa Katibu wa CWT, Japheth Maganga, pia alikataa uteuzi wa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera huku aliyekuwa Makamu wa Rais wa CWT kwa kipindi hicho, Dinah Mathamani, alikubali uteuzi na akaenda katika Wilaya ya Uvinza, mkoani Kigoma.

Uchaguzi huu unatarajiwa kufanyika baada ya kukamilika kwa uchaguzi katika ngazi mbalimbali nchini za chama hicho, kuanzia ngazi za shule (Tawi), wilaya na mikoa. Sasa, chama kinajiandaa kumalizia mchakato wa uchaguzi katika ngazi ya Taifa.

Nafasi nyingine zinazotarajiwa kufanyiwa uchaguzi ni pamoja na katibu mkuu wa CWT, naibu katibu mkuu, mweka hazina, mwakilishi wa walimu wenye ulemavu, mwakilishi wa walimu vijana, mwakilishi wa walimu wanawake, mjumbe wa kamati ya utendaji ya Tucta, wadhamini watatu, na vitengo mbalimbali vya chama.

Ili kupata taarifa zaidi endelea kutufuatilia kupitia website yetu ya www.jembenijembe.com kupitia Instagram ,Facebook, tikok,x zamani twitter pamoja na YouTub


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii