DIRISHA LA KUBORESHA TAARIFA ZA UCHAGUZI KUFUNGWA LEO

Mkurugenzi wa Uchaguzi, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhani Kailima amewataka Watanzania kuitumia siku ya leo Mei 22, 2025 ambayo ni ya mwisho kujiandikisha katika Vituo vya Wapiga Kura ili waweze kupata haki zao za kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025.

Amesema hayo alipotembelea Vituo katika Jimbo la Dodoma Mjini na Mtumba kukagua zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii