Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo May 22, 2025 ameondoka nchini kwenda Japan kumwakilisha Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye maonesho ya World Expo 2025 Osaka.
PM Majaliwa atashiriki pia katika kongamano la biashara, uwekezaji na utalii ambalo litahusisha Wafanyabiashara kutoka Tanzania na Japan na pia atashiriki katika Mikutano ya Uwili yenye lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Japan .
Maonesho hayo yalianza tangu April 13, 2025 na yanatarajia kumalizika October 13, 2025 hii itakuwa mara ya pili kwa Japan (Osaka) kuwa Mwenyeji wa maonesho hayo ya kimataifa, ambapo mara ya mwisho yalifanyika 1970 (EXPO 1970).