MWANAHARAKATI WA KENYA KUACHIWA HURU NA KUREJESHWA NCHINI KWAO

Serikali ya Tanzania imemuachia huru na kutumia usafiri wa gari  kumsafirisha mwanaharakati wa Kenya Boniface Mwangi ambaye sasa amepatikana Ukunda Kaunti ya Kwale nchini Kenya akiwa katika hali ya uchovu mkubwa.

Imeelezwa kuwa Mwangi alikuwa akizuiliwa nchini Tanzania katika mazingira ambayo hayakuwa wazi kabla ya kurejeshwa kwa nguvu kwao kupitia mpaka wa nchi hizo mbili.

Hivyo familia yake imethibitisha kuachiliwa kwake na kueleza kuwa amekimbizwa hospitalini kwa ajili ya uchunguzi wa kiafya.

Hatua hiyo ya kumrejesha imekuja saa chache baada ya serikali ya Tanzania kukumbwa na mashinikizo  kutoka katika Serikali ya Kenya pamoja na wanaharakati wa haki za binadamu waliotaka aachiliwe huru.

Katibu wa Wizara ya Masuala ya Nje ya Kenya Dkt Abraham Korir Sing’Oei siku ya Alhamisi alilalamikia kutoweka kwa Mwangi na kueleza kuwa maafisa wa Kenya walizuiwa kumpata wala kupata taarifa kuhusu hali yake.

Ambapo hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan alitoa kauli ya kuwaonyo  wanaharakati kutoka mataifa jirani huku akisema serikali haitaruhusu mtu yeyote kuvuruga amani ya nchi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii