Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Isihaka Mchinjita anadaiwa kukamatwa na Jeshi la Polisi baada ya kutembelea mradi wa mwendokasi kuangalia kero wanazopitia wananchi.
Kwamujibu wa Taarifa ya iliyotolewa na ofisa habari wa chama hicho, Abdallah Khamis leo Mei 23,2025 alikamatwa alipokuwa akifanya ziara ya kushtukiza katika eneo la Stendi ya Mwendokasi Kimara Mwisho, lengo ikiwa ni kushuhudia namna ambavyo wananchi wanapitia changamoto katika usafiri huo wa umma.
Abdalah amesema baadhi ya viongozi waliojitambulisha ni wafanyakazi wa mradi wa mwendo kasi, walimfanyia fujo kiongozi huyo wakitaka asipokee malalamiko ya wananchi katika kituo cha Kimara kutokana na madhila wanayoyapata katika usafiri huo.