Waislam mkoani Mwanza wamehimizwa kutunza amani wakati huu Nchii inaelekea kwenye uchaguzi mkuu baadae Mwaka huu.
Akitoa hutuba ya ijumaa katika msikiti mkuu wa bakwata mkoa wa Mwanza katibu wa kadhi Ramadhani Khamis amesema ni jukumu la kila muslaam kuhakikisha anailinda na kuitunza amani ya nchii ambayo ni tunu ya Taifa.
Amesema jamii inatakiwa kuwa makini na baadhi ya watu ambao wamekuwa na kauli ambazo zimekuwa zikichochea uvunjifu wa amani na kuwataka viongozi wa dini kusimama na kukemea kauli hizo.
Ameongeza kuwa waislaam wanatakiwa kuzuia viashiria vyenye lengo la kuvunja amani kwani wislaam umehimiza kutangaza amani kwa kila mtu.