ULAJI WA NYAMA NCHINI UMEONGEZEJA KUTOKA KILO 16 HADI 17.6

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amesema kutokana na  kuimarika kwa biashara ya mazao ya mifugo nchini kwa Mwaka 2024/2025 kumechangia kuongezeka kwa ulaji wa mazao ya mifugo ambapo amesema kiwango cha ulaji nyama kimeongezeka kutoka kilo 16 mwaka 2023/2024 hadi kilo 17.6 mwaka 2024/2025 na ulaji wa mayai kutoka mayai 107 mwaka 2023/2024 hadi mayai 119 mwaka 2024/2025.

Waziri Dkt. Ashatu amesema hayo leo May 23,2025 Bungeni Jijini Dodoma wakati akiwasilisha hotuba ya Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2025/2026.

Amessma pamoja na ongezeko hilo, ulaji wa mazao hayo kwa Mtu mmoja mmoja bado haujafikia viwango vinavyopendekezwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) ambayo ni kilo 50 za nyama na mayai 300.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii