ARUSHA MWENYEJI MKUTANO WA 33 WA (SADC)

Mkoa wa Arusha umechaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa 33 wa mwaka wa Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) mkutano unaotarajiwa  kufanyika kesho Mei 26 hadi 31, 2025.

Akizungumza na waandishi wa habari  Mei 25, 2025, mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda amesema mkoa huo umeendelea kuwa kinara kwa mikutano ya kitaifa na kimataifa pamoja na kuwa kitovu cha shughuli za utalii zinazochochea uchumi wa mkoa na Taifa kwa ujumla.

Makonda ameeleza kuwa wakati wa mkutano huo Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Tanzania Jenerali Jacob Mkunda ataongoza majadiliano yatakayolenga kuimarisha ushirikiano wa kijeshi na usalama wa kikanda.

Aidha RC Makonda amewatoa hofu wananchi kuhusu uwepo wa magari ya kijeshi katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Arusha akibainisha kwamba hayo ni maandalizi ya kawaida ya kuhakikisha kunakuwa na ulinzi na usalama wa kutosha wakati wote wa mkutano huo muhimu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii