Jeshi la Uganda limesema nchi hiyo imesimamisha ushirikiano wote wa kijeshi na Ujerumani huku likidai kuwa balozi wa Ujerumani anajihusisha na shughuli za uasi katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
Kufuatia ripoti yakwamba wanadiplomasia kuikosoa tabia ya mtoto wa Rais Yoweri Museveni Muhoozi Kainerugaba ambaye ni mkuu wa jeshi.
Kainerugaba ambaye anatajwa kuwa na uwezekano mkubwa wa kumrithi babake mwenye umri wa miaka 80 kama rais ambaye anajulikana kwa kuandika machapisho yake yenye utata kwenye mitandao ya kijamii.