Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limetoa wito kwa vijana waliomaliza elimu ya kidato cha sita mwaka 2025 kutoka shule zote za Tanzania Bara kujiunga na jeshi hilo kwa mujibu wa sheria mwaka 2025.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Kanali Juma Mrai amesema kuwa vijana hao wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia kesho Mei 28, 2025 hadi Juni 8, 2025.
Kanali Mrai amesema kuwa orodha ya majina ya vijana wote katika makambi ya JKT waliopangiwa na maeneo ya makambi hayo sehemu yalipo pamoja na vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo yapatikana katika tovuti ya JKT: www.jkt.mil.tz
Aidha JKT inawaomba wazazi kuwaruhusu vijana wao ili wahudhurie mafunzo hayo ya jeshi hilo kwa ajili ya kujengewa uzoefu na kujiamini.