Watanzania wametakiwa kuwa wazelendo ili kuilinda nchii kuelekea kipindi cha uchaguzi unaotarajia kufanyika mwaka huu
Hayo yamesemwa na sheikh wa mkoa wa Mwanza Hasani Kabeke wakati akitoa hutuba ya swala ya ijumaa katika msikiti Mkuu wa bakwata mkoa wa Mwanza
Kabeke amesema ni jukumu la kila mtanzania kuhakikisha anakuwa mzalendo kwa Nchii yake, kuwa makini haswa kipindi hiki Nchii inaelekea kwenye uchaguzi mkuu kutoanzisha migogoro ambayo inaweza leta mpasuko kwenye Taifa
Aidha Kabeke amewataka wanasiasa kuwa wazalendo,kwa kufanya siasa safi zisiso za uchonganishi baina ya raia na viongozi wao huku akiwataka vijana kujikita kutafuta kipato,kuwa na maadili na kuacha kutumika na wanasisa kuchafua Nchii yao.
IMEANDIKWA NA MUSTAFA KINKULAH