Mgombea wa nafasi ya Ukurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika kutoka Tanzania Prof. Mohammed Janabi, ametaja vipaumbele saba ambavyo amevinadi mbele ya Mawaziri wa Afya kutoka nchi mbalimbali na wanachama wa Shirika la Afya Duniani katika Bara la Afrika kwa kuomba ridhaa ya kumpitisha kushika nafasi hiyo.
Prof. Janabi amewasilisha vipaumbele hivyo leo May 18, 2025 alipokuwa akijinadi mbele ya Mawaziri hao na kuahidi kuwa endapo atachaguliwa atasimamia uboreshaji wa huduma za afya na kuweka mkazo zaidi kwenye uboreshaji wa huduma za afya ngazi ya msingi “Endapo nitachaguliwa naahidi kusimamia uboreshaji wa huduma za afya kwa wote ili kuweza kufikia malengo endelevu, hadi sasa ni asilimia 46% pekee wanapata huduma bora za afya Afrika huku lengo la kidunia ni kufikia 68% mwaka 2030, pili nitasimamia upatikanaji wa rasilimali fedha za kuwezesha kugharamia upatikanaji wa huduma bora za afy''
Kipaumbele cha tatu alichoainisha ni kuendelea kusimamia utayari wa nchi wanachama katika kukabiliana na majanga pamoja na dharura za afya na amesisitiza pia kuhusu kuboresha huduma za afya ya uzazi kwa Mama na Mtoto pamoja na lishe akisema Afrika inachangia asilimia 70% ya vifo vitokanavyo na uzazi pamoja na 56% ya vifo vya watoto wachanga duniani.
Kipaumbele cha tano amesema ataendelea kuweka msisitizo zaidi kwenye kupambana na magonjwa ambukizi yakiwemo UKIMWI, Kifua Kikuu, Malaria, Magonjwa yasiyoambukiza pamoja na magonjwa yasiyopewa kipaumbele akiswma yanachangia katika kuzorotesha uchumi wa Bara la Afrika, kipaumbele cha sita amesema atasimamia jitihada za kupambana na changamoto ya usugu wa vimelea dhidi ya dawa UVIDA.
Prof. Janabi amehitimsha na kipaumbele cha saba kwa kubainisha kuwa ataimarisha uzalishaji wa bidhaa za afya zikiwemo dawa, vifaa na vifaatiba pamoja na chanjo ndani ya Bara la Afrika.
Kwa taarifa zaidi endelea kutufuatilia kupitia www.jembenijembe.com kwenye Instagram, Facebook, Tikok, x zamani twitter pamoja na YouTube channel yetu ya jembe fmtz