Imeripotiwa hivi karibuni nchini Kenya kukabiliwa na ugonjwa hatari wa KALAZAR, ambapo watu 33 tayari wamekwisha fariki huku visa zaidi ya 1000 vikiripotiwa katika muda mfupi
Hali hii Imeibua maswali namna Afrika inavyoshughulikia magaonjwa, huku mamlaka husika zikiendelea kuchukua hatua zaidi kukabiliana na ugonjwa huo.
Kalazar, au visceral leishmaniasis, ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vya Leishmania, wanaoenezwa kupitia mbu wadogo. Ukiachwa bila kutibiwa, ugonjwa huu unaweza kusababisha vifo kwa zaidi ya asilimia 95%. Aidha, visa vingi vimeripotiwa katika maeneo ya Kaskazini Mashariki mwa Kenya, yakiwemo kaunti za Wajir, Garissa, na Marsabit.
Mary Muthoni, Katibu Mkuu katika Wizara ya Afya, amesema kuwa maambukizi yamefikia 1,041 hadi sasa, na tayari kuna vifo 33, akiongea kwa masikitiko makubwa.
Wizara ya Afya imetuma maabara tatu za rununu na dawa katika maeneo yaliyoathirika, huku wahudumu wa afya wakishirikiana na serikali za kaunti.