Mei 18, 2025 jijini Dar es Salaam kiongozi Mstaafu wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe, alisema amefunguliwa kesi mahakamani na Mfanyabiashara Harbinder Seth ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya (IPTL) akidai kuwa Zitto amemkashifu na kumvunjia heshima mbele ya jamii kupitia chapisho lake kwenye ukurasa wa X (zamani Twitter) kuhusu sakata la IPTL.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Zitto alisema kuwa licha ya Seth kudai fidia ya mabilioni ya fedha yeye haogopi na yupo tayari kwenda mahakamani kusimamia kile alichokiandika huku akisisitiza kuwa ni kweli na kinaakisi hali halisi ya sakata hilo.