Mbunge wa Viti Maalumu, Esther Bulaya ameishutumu Serikali kwa kushindwa kuchukua hatua madhubuti dhidi ya uharibifu unaosababishwa na wanyamapori hususan tembo katika Wilaya ya Bunda mkoani Mara.
Amesema hayo wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa fedha 2025/26 iliyowasilishwa leo Jumatatu Mei 19, 2025 bungeni jijini Dodoma na waziri wa wizara hiyo, Dk Pindi Chana Bulaya ameleza kuwa zaidi ya wananchi 1,400 hawajalipwa fidia kutokana na madhara yaliyosababishwa na tembo kwa zaidi ya miaka miwili.
Amefafanua kuwa zaidi ya ekali 5,390 zimeteketezwa na ng’ombe zaidi ya 800 wameuawa. Leo tunataka wananchi wa Bunda waone kwamba kuwa na mbuga siyo tena fahari bali ni mzigo,” amehoji Bulaya.
Mbunge huyo alieleza kuwa licha ya kuwa Wilaya ya Bunda iko jirani na maeneo ya hifadhi, bado hakuna jitihada za maana zinazochukuliwa kulinda maisha na mali za wananchi wanaoishi pembezoni mwa hifadhi hizo na hawashirikishwi vya kutosha hata panapokuwa na mabadiliko huku akitolea mfano wa uhamishaji wa makaburi.
Ili kupata taarifa zaidi endelea kutufuatilia kupitia website yetu ya www.jembenijembe.com kupitia Instagram ,Facebook, tikok,x zamani twitter pamoja na YouTube