Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mamlaka ya umma inayohusika na masuala ya afya imesema maambukizo ya mpox yameanza kupungua.
Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni, DRC ilisajili visa vipya 182 wiki iliopita na kufikisha idadi ya maambukizo yalioripotiwa tangu mwezi Januari tarehe moja mwaka wa 2024 kuwa 21,452.
Idadi kubwa ya visa hivi viliripotiwa katika jiji kuu la Kinshasa, ambalo peke lilisajili maambukizo mapya 88 katika kipindi cha wiki moja, visa vingi vikitokea kwenye magereza.
Visa 30 vimeripotiwa katika gereza la kijeshi la Ndolo jijini Kinshasa kikiwemo kifo kimoja.