Vijana zaidi ya 1,000 kutoka wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza wamefanya matembezi ya zaidi ya kilomita 30 kutoka ofisi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Sengerema kuelekea Kata ya Busisi kushuhudia Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua daraja la kihistoria la JP Magufuli Kigongo - Busisi leo Juni 19 2025.
Katibu wa UVCCM mkoa wa Mwanza, Cde. John Madagaa na Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Sengerema, Cde. Patrick Mundeba wameongoza matembezi hayo yenye lengo ka kumpongeza Rais Samia kwa kukamilisha mradi huo wa daraja la Kigongo - Busisi lenye urefu wa kilomita 3 ambalo alilipokea mwaka 2021 likiwa limefikia asilimia 25 na sasa limekamilika kwa asilimia 100 na kutekeleza vyema Ilani ya CCM ya 2020-2025.
Vijana hao wamewakaribisha vijana wote nchini kujumuika nao katika uzinduzi huo huku wakibeba ujumbe mzito kwa dunia kuwa Oktoba Tunatiki.