Kufuatia na usomwaji wa bajeti kuu serikali katika nchi tofauti tofauti ikiwemo Tanzania, Rwanda, Kenya, na Uganda kuwasilisha bajeti zao za kitaifa, huku zikionesha vipaumbele vyao vya kiuchumi na mipango ya maendeleo nchi.
Katika eneo hili, Kenya inasimama kama kinara mkubwa, huku bajeti yake ya 2025/2026 ikiiwa kubwa pengine zaidi ya Uganda na Tanzania zikiunganishwa. Mataifa haya yamepanga kuongeza matumizi kwa jumla ya dola bilioni 5 katika kipindi cha miezi 12 hadi Juni 2026, ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Bajeti ya Uganda inaonekana zaidi kuelekezwa kwenye masuala ya uchaguzi, ikiwa na matumizi makubwa kwenye usalama na utawala, ikionesha vipaumbele tofauti vya kitaifa.
Bajeti ya Tanzania yenyewe haijaja na miradi mikubwa, imebaki kuendeleza miradi mikubwa ya kimkakati inayoendelea ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR na miundombinu ya barabara ya mwendo kasi katika jiji la Dar es salaam.
Kwa ujumla mataifa ya Afrika yanaendelea kujitahidi kufikia utulivu wa kiuchumi na maendeleo, huku bajeti za kitaifa zikicheza jukumu muhimu katika kuunda sera na vipaumbele.
Aidha kutokana na sababu hizo haya ni mataifa 10 Bora barani Afrika kwa bajeti kubwa kitaifa mwaka 2025/2026
1. Afrika Kusini - Dola bilioni 141.4
Afrika Kusini inaongoza kwa bajeti kubwa zaidi barani Afrika kwa mwaka 2025, ikiwa na ugawaji wa kuvutia wa dola bilioni 141.4. Bajeti ya nchi hiyo inaipa kipaumbele miundombinu, huduma za kijamii, na maendeleo ya kiuchumi.
2. Algeria - Dola bilioni 126
Algeria inafuata kwa karibu ikitenga bajeti ya dola bilioni 126, ikionesha uwekezaji mkubwa katika sekta ya nishati na ulinzi.
3. Misri - Dola bilioni 91
Misri inashika nafasi ya tatu kwa dola bilioni 91, ikielekeza fedha kwenye elimu, afya, na miundombinu ya umma.
4. Morocco - Dola Bilioni 73
Morocco pia inaonekana wazi katika orodha hii, ikiwa na bajeti ya kitaifa ya dola bilioni 73.
5. Angola - Dola bilioni 37.847
Angola inashika nafasi ya tano na bajeti ya dola bilioni 37.847, hasa ikichangiwa na mapato yake ya mafuta.
6. Nigeria - Dola bilioni 36.7
Nigeria, taifa lenye idadi kubwa zaidi ya watu barani Afrika, lina bajeti ya dola bilioni 36.7, likilenga kubadilisha uchumi na miundombinu.
7. Kenya - Dola bilioni 32.65
Kenya inafuata na bajeti ya dola bilioni 32.65, ikipa kipaumbele elimu, afya, na ukuaji wa uchumi. Kama ilivyoelezwa, bajeti hii inazidi kwa mbali zile za majirani zake wa Afrika Mashariki, Uganda na Tanzania.
8. Libya - Dola bilioni 26
Libya, licha ya changamoto za kisiasa, inaendelea kudumisha bajeti ya dola bilioni 26.
9. Ivory Coast - Dola bilioni 25.22
10. Tunisia - Dola bilioni 25.16
Ivory Coast na Tunisia zinamalizia orodha ya mataifa kumi bora, zikiwa na bajeti za dola bilioni 25.22 na dola bilioni 25.16 mtawalia, zote zikilenga kukuza utulivu wa kiuchumi na maendeleo.
Bajeti hizi za kitaifa za 2025 zinasisitiza dhamira ya Afrika katika ukuaji wa uchumi, upanuzi wa miundombinu, na maendeleo ya kijamii. Huku nchi zikikabiliana na changamoto kama vile mfumuko wa bei, usimamizi wa deni, na kuyumba kwa kisiasa, ugawaji huu wa bajeti utakuwa muhimu katika kuunda mandhari ya kiuchumi ya baadaye ya bara hili.