Mechi za Mzunguko wa pili AFCON 2025 kuendelea hii leo

Mechi ya awali kabisa hii leo ni kati ya Angola dhidi ya  Zimbabwe timu hizi za kundi zinakutana baada ya kila mmoja kuchapwa katika mechi zao za mzunguko wa kwanza huku vigogo Misri watapambana dhidi ya Afrika Kusini.

Michuano ya kandanda ya mataifa barani Afrika AFCON 2025 inaendelea hii leo kwa mechi za mzunguko wa pili katika viwanja mbalimbali nchini Morocco.

Aidha mechi ya awali kabisa hii leo ni kati ya Angola dhidi ya Zimbabwe timu hizi za kundi zinakutana baada ya kila mmoja kuchapwa katika mechi zao za mzunguko wa kwanza ambapo baadaye jioni kutakuwa na mechi mbili za kundi hilo hilo kati ya vigogo Misri dhidi ya Afrika Kusini. 

Hata hivyo mechi za kundi A mechi ya awali itakuwa kati ya Zambia Chipolopolo ambao watamenya na visiwa vya Comorro,  mechi ya usiku na ya mwisho itawakutanisha wenyeji Morocco dhidi ya Mali.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii