Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wabunge baadaye leo Jumatatu wanatarajiwa kupiga kura, kuamua hatima ya Spika Vital Kamerhe, baada ya siku kadhaa za vikao ambavyo vimekuwa vikifanyika kujadili utendakazi wake.
Wabunge wanatarajiwa kufanya uamuzi huo, baada ya siku ya Ijumaa na Jumamosi iliyopita, Kamerhe kufika mbele ya Kamati maalum iliyoundwa, chini ya uenyekiti wake Peter Kazadi, kutoka cha cha UDPS, inayomchunguza.
Washirika wa karibu wanasema, hakuna ushahidi uliopatikana kumpata Kamerhe ambaye ni mshirika wa karibu wa rais Felix Tshisekedi na hatia.
Aidha, wamedai kuwa baadhi ya sahihi za wabunge, hazikuwa halali, akiwemo mtu mmoja ambaye sio mbunge, aliyeruhusiwa kushiriki kwenye mchakato wa kutaka kumwondoa Spika Kamerhe kwenye nafasi yake.
Hata hivyo, wabunge watanao wanaodaiwa kutotia saini mswada dhidi ya spika Kamerhe, walithibitisha kuwa saini hizo ni zao, na sasa Kamati hiyo inasuburiwa kuwasilisha ripoti yake na baadaye wabunge kupiga kura dhidi ya Kamerhe kuanzia saa 10 jioni saa za Kinshasa kuamua hatima ya Kamerhe.