Vital Kamerhe, Spika wa Bunge la taifa, ajiuzulu

Spika wa Bunge la taifa nchini DRC, Vital Kamerhe, amejiuzulu. Alikuwa mada ya ombi ambalo lilipaswa kupigiwa kura wakati wa kikao cha mashauriano katika makao makuu ya Baraza la Wawakilishi mjini Kinshasa. Hatimaye, amewasilisha barua ya kujiuzulu kwake kwa Kongamano la viongozi, ambalo huwaleta pamoja viongozi wa makundi ya wabunge, kulingana na wabunge kutoka chama chake, UNC.

Vital Kamerhe amejiuzulu wadhifa wake kama Spika wa Bunge la taifa siku ya Jumatatu alasiri, Septemba 22. Kulingana na vyanzo kadhaa katika Baraza la Wawakilishi, ikiwa ni pamoja na wabunge walionukuliwa na Radio Okapi, amewasilisha barua ya kujiuzulu kwake kwa kongamano la viongozi kutoka makundi mbalimbali ya wabunge.

Vital Kamerhe amejiuzulu wadhifa wake Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Uamuzi huu unakuja baada ya siku kadhaa za mvutano uliochochewa na ombi lililowasilishwa na wabunge kutoka chama cha rais cha UDPS na vyama vingine, wakimtuhumu kwa utovu wa usimamizi na kuzuia usimamizi wa bunge.

Walalamikaji walimkosoa Kamerhe kwa kukosa kuafikiana na vipaumbele vya serikali, haswa usimamizi usio wa wazi wa pesa za bunge. Licha ya majaribio yake ya kutuliza hali, Kamerhe alishindwa kupata uungwaji mkono wa kutosha. Baadhi ya waangalizi wanaona hili kama suluhu la ndani la matokeo ndani ya Muungano Mtakatifu, unaolenga kuimarisha udhibiti wa UDPS kwenye taasisi hiyo.

Kujiuzulu kwa Kamerhe kunafungua njia ya uchaguzi wa haraka wa ofisi mpya ya Bunge, chini ya uongozi wa muda wa Naibu Spika Isaac Tshilumbayi. Mustakabali wa Bunge la taifa haujulikani, na nafasi hii inaweza kuibua mijadala kuhusu mageuzi ya kitaasisi na mapambano dhidi ya kutokujali.

Wakati kikao cha mashauriano kikiitishwa kuchunguza ripoti ya Tume Maalumu iliyoundwa kuchunguza malalamiko dhidi ya wajumbe 5 wa ofisi hiyo, akiwemo Vital Kamerhe mwenyewe, bado kinasubiriwa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii