MGAMBO WATAKIWA KUSHIRIKISHA POLISI KUTATUA CHANGAMOTO ZA KIUTENDAJI.

Polisi Kata ya Liganga iliyopo Wilaya ya Songea Vijijini mkoani Ruvuma Mkaguzi wa Polisi (INSP) Datius Dioniz Septemba 23, 2025 amefanya kikao kazi na Askari Mgambo pamoja na Sungusungu wa kijiji cha Liganga kwa lengo la kujadili mambo mbalimbali ya kiutendaji ili kuhakikisha wanaendelea kutekeleza majukumu yao ya Ulinzi kwa kuzingatia sheria za nchi ili wananchi waendelee kufanya shughuli zao kwa amani na utulivu muda wote bila malalamiko yoyote yanayotokana na utekelezaji wa majukumu bila kufuata misingi ya sheria.

Mkaguzi huyo aliwaambia askari hao kuwa kila mmoja kwa nafasi yake inabidi awajibike ipasavyo katika kutekeleza majukumu ya Ulinzi na Usalama bila kusahau kushirikisha Jeshi la Polisi kupitia kwa Polisi kata aliye katika eneo lake pale unapokumbana chamgamoto inayohusiana na masuala ya Ulinzi na Usalama ili iweze kutatuliwa kwa kuzingatia kanuni, taratibu na sheria za nchi yetu.

Sambamba na hilo pia INSP. Dioniz aliwataka askari hao kuwa mstari wa mbele katika kuwaelimisha wananchi kuhusiana na masuala ya Ulinzi na Usalama ili waweze kupata uelewa na kushiriki vyema katika Ulinzi wa maeneo yao kupitia vikundi vya Ulinzi shirikishi na kuwataka kuepuka tabia ya kujichukulia sheria mkononi pale wanapokamata wahalifu badala yake wawafikishe maeneo husika ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.

Aidha amewasisitiza askari hao kuendelea kufanya doria na misako katika maeneo yao ili kuhakikisha Usalama unaimarika katika kipindi hiki cha Kampeni za Uchaguzi Mkuu sambamba na kuwahamasisha wananchi wanaomiki silaha kinyume na sheria na kuwataka kusalimisha silaha hizo mapema kabla ya muda wa msamaha wa kusalimisha sila wa kutoshtakiwa kuisha ambapo tarehe ya mwisho ya usalimishaji ni Oktoba 31, 2025.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii