Baraza la Madiwani Rungwe Lawafuta Kazi Watumishi Watatu kwa Utoro

Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya limeazimia kuwafuta kazi watumishi watatu wa halmashauri hiyo kwa tuhuma za utoro wa muda mrefu kazini.

Uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha baraza hilo baada ya kujadili mashauri ya kinidhamu yaliyowasilishwa mbele ya madiwani.

Akitoa ufafanuzi kuhusu maazimio hayo, Mwenyekiti wa Halmashauri, Ndg. Gabriel Mwakagenda, amesema jumla ya mashauri manne yaliwasilishwa katika kikao hicho, ambapo mashauri matatu yalihitimishwa kwa uamuzi wa kufutwa kazi kwa watumishi husika, huku shauri moja likirejeshwa ili kuanza upya utaratibu wa kisheria.

Mwakagenda amewasihi watumishi wa umma waliokabidhiwa dhamana ya kuwatumikia wananchi kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya utumishi wa umma, akisisitiza kuwa uzembe na utoro havitavumiliwa.

Amesema halmashauri itaendelea kusimamia nidhamu kazini ili kuhakikisha huduma bora zinawafikia wananchi kwa wakati na kwa ufanisi.

Sasa ili kupata undani wa  taarifa hii tafadhali usikose kutufuatilie na Usikilize jembe Habari Kamili hapo saa saba kamili mchana  ambapo msomaji wetu wa hii leo ni @georgekivumbi tafadhali usipitwe na taarifa zetu Mahiri kabisa. 

Lakini pia tembelea mitandao yetu ya kijamii ya Jembefmtz

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii