Watu 13 wamefariki na wengine 57 kujeruhiwa kufuatia mlipuko mkubwa uliosababishwa na moto katika kambi ya kijeshi nchini Burundi.
Jeshi limesema moto huo ulizuka usiku katika ghala la kuhifadhia vifaa vya kijeshi na kusababisha milipuko kadhaa baada ya risasi na mabomu kulipuka.
Msemaji wa jeshi, Gaspard Baratuza, amesema chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme, akisisitiza kuwa hakukuwa na shambulio lolote dhidi ya kambi hiyo.
Tukio hilo lilitokea katika eneo la Musaga, nje kidogo ya jiji la Bujumbura, ambapo wakazi walikimbia kwa hofu huku milipuko ikisikika kwa umbali mkubwa.
Maafisa wamewataka wananchi kutoa taarifa kuhusu mabaki ya milipuko ambayo hayajalipuka, wakati hali ikianza kurejea kawaida.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime