Manuel Neuer arejeshwa timu ya Taifa ya Ujerumani

Kipa mkongwe wa Timu ya Taifa ya Ujerumani, Manuel Neuer amerejeshwa kutoka kustaafu na kujumuishwa kwenye kikosi kitakachoshiriki Kombe la Dunia.

Neuer mwenye umri wa miaka 40 alikwishatangaza kustaafu soka la kimataifa baada ya michuano ya Euro 2024, lakini amerejeshwa na kocha Julian Nagelsmann katika kikosi chenye wachezaji 26 kwa ajili ya michuano hiyo itakayofanyika Canada, Mexico na Marekani.

Uamuzi huo umemuondoa Oliver Baumann kutoka Klabu ya Hoffenheim, kwenye nafasi ya kipa namba moja, licha ya kuwa matumaini ya kuanza katika kikosi cha kwanza.

Nagelsmann amesema kurejea kwa Manuel Neuer ni pigo kwa Baumann, lakini amesisitiza kuwa uzoefu mkubwa wa kipa huyo aliyecheza mechi 124 za kimataifa umechangia uamuzi huo.

Shinikizo la kumrejesha Neuer liliongezeka baada ya kuonyesha kiwango bora akiwa na Bayern Munich, hasa katika mechi za robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii