Kiongozi mkongwe wa upinzani nchini Uganda anayezuiliwa jela Kizza Besigye ambaye hapo jana alianguka akiwa mahakamani, amelazwa hospitali akiwa katika hali mbaya.
Kiongozi mkongwe wa upinzani nchini Uganda anayezuiliwa jela Kizza Besigye ambaye hapo jana alianguka akiwa mahakamani, amelazwa hospitali akiwa katika hali mbaya.
Mkewe Winnie Byanyima ameandika kwenye ukurasa wa X hivi leo kwamba Besigye mwenye umri wa miaka 70 amelazwa katika chumba maalum cha wagonjwa mahututi akiwa amepoteza fahamu katika hospitali ya rufaa ya Mulago. Jana Jumatano mwanasiasa huyo mkongwe mkosoaji mkubwa wa serikali ya rais Museveni alifikishwa mahakamani mjini Kampala kujibu kesi inayomkabili ya uhaini.
Amekuwa akishikiliwa jela tangu Novemba mwaka 2024 ambapo mawakili wake,wafuasi na wanaharakati wa Haki za binadamu wanasema tuhuma mashtaka yanayomkabili yamechochewa kisiasa na hatua ya kumzuilia jela ni sehemu ya mpango unaoendelea wa kuwaandama wapinzani nchini Uganda wa rais Museveni.